Serikali ya Sudan Kusini
imeelezea kwa mara ya
kwanza kuhusu idadi kubwa ya wanajeshi wake wanaoasi jeshi na kujiunga na waasi
wanaoongozwa na makamu wa zamani wa Rais Riek Machar..........
Serikali hiyo imeelezea hayo ikitaka jamii ya kimataifa kuisaidia kwa kutuma wanajeshi nchini humo ili kujaza pengo hilo.
Kinara wa serikali Tulklio Odongi aliambia bunge siku ya Jumatatu kuwa hadi asilimia sabini ya wanajeshi wa serikali wanageuka na kuwa watiifu kwa Riek Machar pamoja na kuasi jeshi.
Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati na kutuma vikosi vya usalama hadi pale udhaifu huo utakapokwisha.
Bwana Odongi alimsihi Rais Salva Kiir kuhakikisha kuna ulinzi wa kutosha wa Ardhini, angani na majini ili kundoa wasiwasi unaosababishwa na wanajeshi wa serikali kuasi jeshi.
Kuna taarifa kuwa serikali ya Sudan Kusini inafadhili jeshi la Uganda ili kuisaidia na kupambana dhidi ya waasi.
Wakati huohuo, waasi wa Sudan Kusini wamekiri kuwa wanajeshi wanaasi jeshi na hata kuonya kuwa wanajeshi zaidi wanajiandaa kuhamia upande wa waasi.
Upande wa Riek Machar unasema kuwa jeshi limekuja kujionea kuwa Rais Salva Kiir ndiye anayechochea vita huku akisababisha mapigano yasiyo na msingi hata kidogo.
0 maoni:
Post a Comment