Maafisa wa polisi wamewakamata watu
1000 wanaoshukiwa kuwa katika vuguvugu moja linalolaumiwa kwa jaribio la
mapinduzi ambalo halikufaulu 2016.
Uturuki inasema kuwa vuguvugu linalomtii kiongozi wa kidini Fethulah Gullen lilipanga mapinduzi hayo ya Julai 2016 ili kuiangusha serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan.
Mapema mwezi huu rais wa taifa hilo alishinda kura ya maoni kuhusu kuimarisha mamlaka yake.
Kutokana na ushindi huo mwembamba rais Erdogan anaweza kuwa rais mwenye mamlaka hatua inayomuongezea mamlaka katika wadhfa wa urais ambao haukuwa na uwezo.
Maimamu 1,009 katika mikoa 72 wamekamatwa na wanazuiliwa kufikia sasa, kulingana na waziri wa maswala ya ndani Suleyman Soylu, ambaye aliripotiwa akiitaja kuwa hatua muhimu ya Uturuki.
Orodha ya takriban watu 3,224 ilikuwa imewekwa na maafisa wa polisi katika operesheni ya mikoa 81,ripoti ilisema.
Katika mji mkuu wa Istanbul pekee, washukiwa 390 walikuwa wakitafutwa.
Ilitarajiwa kwamba msako wa walioshiriki katika mapinduzi hayo utaendelea baada ya rais kupata ushindi aliohitaji katika kura ya maoni ili kujiongezea mamlaka
Anajihisi amepata nguvu na licha ya upinzani kupinga matokeo ya kura hiyo rais amesema kuwa matokeo hayo ndio rasmi na hakuna lolote jingine litakalofanyika.
Na ilipofikia siku ya Jumatano kikosi cha polisi kilikabiliwa na msako na taasisi nyengine zinatarajiwa kufanyiwa msako huo pia.
Chama tawala cha AKP kilikuwa kimejaa wafuasi wa Gullen wakati rais Erdogan alipokokuwa mwandani wake wa karibu.
0 maoni:
Post a Comment