TFF
LEO: Simba Oljoro waingiza mil 40, mtihani wa mawakala
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
NCHINI KUFANYIKA MACHI 29, 2012
Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Machi 29 mwaka huu saa 10 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.
Muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90. Mtihani uliopita ulifanyika Septemba 29 mwaka jana ambapo watahiniwa wanane walijitokeza na kufanya mtihani huo.
Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.
SIMBA, OLJORO JKT ZAINGIZA MIL 40
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa Februari Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,191,000.
Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 105 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A walikuwa 11,860.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 7,023,171, uwanja sh. 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 936,423, TFF sh. 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 234,106.
Nayo mechi namba 104 kati ya African Lyon na Polisi Dodoma iliyochezwa Februari Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 45,000 kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 6,864.41 kila timu ilipata sh. 2,591, Uwanja sh. 514, TFF sh. 514, DRFA sh. 205, FDF sh. 257 na BMT sh. 51.

0 maoni:
Post a Comment