Penzi la kweli lina upendo wa dhati ulio ndani ya wapenzi wawili,
penzi hili limejaa huruma kwa wapendanao,
Penzi la aina hii wapendanao mioyo yao hujaa woga kwa kuhakikisha
wanakuwa watu wa furaha na utumia muda wao mwingi wakiwa pamoja
kubuni mbinu kuhakikisha mwenza wake hajihisi upweke.
Watu wa kundi hili huwa wavumilivu kwa hali yoyote na ujitoa muhanga kwenye
matatizo pia huogopa wao kuwa vyanzo vya matatizo.
Huwasikiliza wapenzi wao kuliko mtu yeyote hata wazazi wao.
Hulifurahia penzi kuliko kitu chochote,
hata kama hawana kitu wao upendo ni shibe ya mioyo yao.
Ni wepesi kusamehe na kusahau maudhi kwa haraka hawapendi
kujikumbusha maudhi yalioukeresha moyo wao.
0 maoni:
Post a Comment