Sitaki mnyimane
Makala ya leo itajikita katika kuwakemea na hata
kuwalaani
wale wote wanaotumia tendo la ndoa kama
siraha ya
kuwaangamiza wenzao kwa kuwanyima haki zao za msingi
katika ndoa.
Miongoni kwa haki hizo ni tendo la ndoa – unyumba.
Kinachowaunganisha watu kuwa wapenzi, wachumba na
hata
kufikia kuwa wanandoa ni tendo la ndoa. Mara
nyingi pasipokuwa na tendo la ndoa
na mapenzi hakuna,
hata ndoa huvunjika. Nani anabisha?
Ndoa nyingi zimevunjika kutokana na mmoja
wa wanandoa
kupatwa na maradhi yaliyosababisha
kuondoa uweze wake wa kutenda tendo la ndoa.
Sasa inakuwaje wale wanandoa walio wazima
wanyimane utamu huo kwa nia ya
kukomoana?
Yaani kuna baadhi ya wanandoa wao wakikosana
kidogo tu
basi mmoja huamua kumnyima unyumba
mwenzake. Wahenga walisema vikombe
vilivyowekwa
kabatini ambavyo havina hata akili huwa vinagongana,
itakuwaje kwa
binaadamu wanaoishi pamoja.
Kwa watu mnaoishi pamoja lazima kutakuwa na siku
‘watapishana kauli,’ watagombana kwa sababu yoyote ile.
Kwani sababu za
kugombana zipo nyingi,
inategemea tu na mtu anavyoyachukulia makosa
ya
mwenziwe. Maana hakuna mtu asiyefanya kosa.
0 maoni:
Post a Comment