Mambo matatu kwa wasuluhishi wa ndoa
1. Mapenzi si msiba ila yanaliza
Kwa msuluhishi yeyote ni muhimu kufahamu kwamba,
mapenzi si msiba lakini kuna wakati yanaliza.
Mapenzi yanaliza kwa njia mbili; moja ni machozi ya
furaha yanayomtoka mtu kwa pendo la dhati kwa mwenzake.
2. Aliyekosewa huwa na jazba
Ni jambo muhimu sana kulijua msuluhishi.
Kwamba mtu aliyekosewa na mumewe au na
mkewe huwa na jazba, haswa kwa wale wenye kupigwa.
Msuluhishi lazima aelewe mtu kupigwa na mumewe au
mkewe kunauma zaidi kuliko kupigwa na mtu yeyote.
3. Epuka kutoa amuzi la kuachana
Huu ni mwiko kwa msuluhishi kuwaamuru wanandoa
waachane kutokana na kutofautiana kwa namna yoyote.
Siku zote ukipewa jukumu la kusuluhisha ndoa neno
“achaneni” usiende nalo kwenye kikao. Hutakiwi kutoa
ushauri wa aina hii. Suluhisha jinsi unavyoweza ukishindwa
waachie wenyewe.
0 maoni:
Post a Comment