USHAURI
KIKWAPA CHAWEZA KUVUNJA NDOA
MADA ya
leo katika safu hii inahusu umuhimu
wa usafi katika kuimarisha penzi. Usafi ni
kichocheo muhimu kinachoweza kuimarisha
uhusiano bora katika mapenzi.
Lakini
uchafu na hasa wa kikwapa ni sumu na
chanzo mojawapo kikubwa kinachoweza
kutenganisha penzi. Ninaposema kikwapa
namaanisha uchafu. Nikisema mtu mwenye
kikwapa namaanisha mtu mchafu.
Najua, si kila mtu anayenuka kikwapa ni
kwa sababu ni
mchafu. Wapo ambao
hujitahidi kuoga kila baada ya muda
mfupi ili kudhibiti
kikwapa hali inayotokana na
jasho linalonuka.
Kwa hiyo, kwa mtu msafi dawa ya kwanza ya
kudhibiti
kikwapa ni kuoga mara kwa mara na
dawa ya pili ni kupaka mafuta yanayonukia a
u
kupulizia utuli (pafyumu).
Mtu ambaye hajitambui kuwa ana kikwapa na
hivyo
akajiachia tu, haogi mara kwa mara na
hataki kutumia marashi atakuwa na hasara
kubwa
katika mapenzi kwa sababu ya ‘uchafu’ huo.
Kuna watu
wanapendwa kutokana na usafi wao tu.
Si pesa wala elimu. Hata uzuri hawana,
lakini kila
wakati utawaona wako safi, watanashati na wenye mvuto.
Mwili safi,
nguo safi na ukimfuatilia utagundua hata
mazingira anayoishi yako safi.
Wapo
wengine wazuri wa sura na umbo lakini kutokana na
uchafu wao uzuri wote unamezwa
na kikwapa.
Thamani ya uzuri wao haionekani tena kutokana na kikwapa.
Tabia ya
mtu kuwa msafi au mchafu haijifichi. Ukitaka
kujua mazingira ya mtu anavyoishi
nyumbani kwake
mwangalie akiwa mtaani.
Ukimwona
mtaani yuko ‘rafu rafu’ muda wote ujue
hata nyumbani kwake yuko hivyo. Ukimwona
msafi na
muda wote yuko ‘smati’ hata kwake anakuwa hivyo.
Kikwapa
kinadhibitika lakini kisipodhibitiwa
mwenye kikwapa ajue kuwa kinapunguza
hamasa
ya mapenzi. Kwa mwanamke au mwanaume msafi
inakuwa vigumu kwake kuwa na
mahusiano bora na
mpenzi mwenye kikwapa. Hawaendani.
0 maoni:
Post a Comment