Msichana muogeleaji wa China Ye Shiwen hajatumia dawa kwenye michezo, mwenyekiti wa Kamati ya Olympiki Uingereza. Amesema hayo baada ya kocha wa Marekani kuonyesha wasiwasi wa kuvunja kwake rekodi ya dunia katika mshindano ya kuogelea.
Mwenyekiti huyo Lord Colin Moynihan amesema Ye, mwenye umri wa miaka 16, alipitia hatua zote za kupimwa kama anatumia dawa hizo na kukutwa kuwa ni safi na anastahili kutambuliwa kwa kipaji chake.Ye alivunja rekodi yake mwenyewe kwa sekunde tano katika mita 400 Medley.
0 maoni:
Post a Comment