Rais wa Uganda Yoweri Museveni
amewataka watu kuepuka kugusana moja kwa moja baada ya virusi hatari vya Ebola
kuenea katika mji mkuu Kampala.
Watu
kumi na wanne wamekufa akiwemo mmoja mjini Kampala, tangu kuzuka kwa ugonjwa
huo magharibi mwa Uganda wiki tatu zilizopita, alisema katika taarifa maalum
kwa Taifa.
Ebola
ni moja ya magonjwa hatari duniani.
Unaenea
kwa kugusana na unaua mpaka 90% ya watu walioambukizwa.
Bw
Museveni alisema maafisa wa afya wanajaribu kufuatilia kila mmoja ambaye ana
waathirika ili kwamba waweze kuwekewa Karantini.
Watu
hawana budi kuepuka kuepeana mikono, kubusiana au kufanya mapenzi kuzuia kuenea
kwa ugonjwa huo, aliongeza.
Bw
Museveni alisema ndugu na amrafiki wasimzike mtu yeyote anayehisiwa kuwa
amekufa kwa Ebola.
0 maoni:
Post a Comment