JESHI LA MISRI LATUMIA WAANDAMANAJI
![]() |
| wanajeshi wakiwa mitaani nchini misri pamoja na waandamanaji |
Wanajeshi nchini Misri wameanza
kuwaondoa watu kutoka katika eneo la ikulu ya rais mjini Cairo ambako kumekuwa
na makabliano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi
Limetuma vifaru na magari mengine
yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha
kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia matukio wanasema kuwa
waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo.
Makabiliano yamesababisha vifo vya
watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.

0 maoni:
Post a Comment