TANZANIA KUSIMAMIA WANAJESHI WA PAMOJA DRC
![]() |
| Picha ya Rais wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa SADC |
![]() |
| Raiya wa DRC wakiwa mitaani na watoto wadogo wakiangaika kutokana na machafuko nchini humo |
Waziri wa Ulinzi wa DR Congo, Dakta
Crispus Kiyonga amethibitisha uundwaji wa jeshi hilo, akisema litafanya kazi
chini ya usimamizi wa Tanzania.
Mapigano ya hivi sasa mashariki mwa
Congo yalizuka mwezi Aprili mwaka huu wakati waasi wa M23 walipoliasi jeshi la
nchi hiyo na kusababisha watu laki tano kuyakimbia makaazi yao wakihofia
usalama wao.
Wakati huohuo, viongozi wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC, wameanza
mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini Tanzania.
Wameanza kwa kufanya kikao cha Asasi
ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA chini ya
Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.


0 maoni:
Post a Comment