WAANDAMANAJI 10 WAUWAWA NA
WANAJESHI
![]() |
| Baadhi ya Wanajeshi wa Sudani Kusini wakiwa na zana za kijeshi |
Umoja wa Mataifa unasema kuwa jeshi
la Sudan Kusini limewapiga risasi na kuwauwa watu 10, ambao walikuwa
wakiandamana kupinga kuhamishwa kwa makao makuu ya serikali za mitaa magharibi
mwa nchi.
Afisa wa kuweka amani wa Umoja wa
Mataifa huko Bahr el-Ghazal amesema watu wane waliuwawa katika mji wa Wau
kwenye mapambano ya jana usiku.
Na wengine sita waliuwawa baada ya
kukusanyika kulalamika juu ya mauaji ya awali.
Jeshi la Sudan Kusini limekataa
kusema kitu.

0 maoni:
Post a Comment