MKUTANO WA HALI YA HEWA WASOGEZWA
MBELE
Mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya
hewa umeendelea ingawa ukitarajiwa kumalizika Ijumaa.
Kumetokea mabadiliko jana usiku na
kuna uwezekano wa mataifa tajiri kutakiwa kuzilipa nchi masikini kwa hasara
inazopata kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Marekani imepinga vikali hatua
zilizopendekezwa - inasema gharama zake zitakuwa hazina kikomo.
Lakini baada ya mvutano katika
majadiliano ya usiku kucha, swala la "Hasara na Uharibifu" sasa liko
katika sehemu ya mwisho ya majadiliano.
Nchi ndogo za visiwa ambazo
zinakabili hatari ya kugubikwa na maji, zinasema zitatoka kwenye mkutano huo
unaofanywa Doha, Qatar, iwapo Marekani itapiga kura kukataa makubaliano
yanayopendekezwa.
Kisiasa makubaliano hayo ni muhimu
sana.
Msimamo wa Umoja wa Ulaya bado
haujulikani wazi.
Marekani inataka iungwe mkono na
mataifa mengine yanayofanya uharibifu mkubwa wa mazingira, kama Canada.
Mataifa kama hayo yanaweza kubeba
mzigo mkubwa wa kulipa fidia kwa uharibifu huo.
Ikiwa Marekani itaachwa peke yake
kupambana na makubaliano hayo, basi wajumbe wake watakuwa na mtihani mkubwa.
Ama wakubali kauli ya wengi na
wakiri kuwa mataifa yaliyosababisha mabadiliko ya hewa yawajibike kwa nchi
nyengine zinazoumia, au wakatae kutia saini.
Iwapo Marekani itapinga makubaliano
basi Rais Obama ataonekana kuwa ameshindwa na hana msimamo thabiti kwa sababu
wakati wa kampeni za uchaguzi aliahidi kuwa atashughulikia mabadiliko ya hali
ya hewa.
Na akikubali makubaliano wapinzani
wake wa chama cha Republican watamshutumu kuwa anayapa kipa umbele makubaliano
yatayoumiza uchumi wa Marekani.

0 maoni:
Post a Comment