Watu wanane wamekufa baada ya nyumba
kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi
mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya
ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la
Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha
Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa
kwamba miili miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa
mapema leo.
Watu wengi
hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na
maporomoko ya ardhi.
0 maoni:
Post a Comment