MADDONA ANATAKIWA KUSEMA UKWELI ‘MALAWI’
MADONNA akiwa nchini Malawi |
Malawi, imemtuhumu muimbaji wa Marekani Madonna kwa kuwadhulumu maafisa wa serikali baada ya kulalamika kuhusu alivyopokelewa alipoizuru nchi hiyo.
Madonna ambaye ameasili watoto wawili kutoka Malawi , alizuru shule kumi ambazo anazifadhili nchini humo hivi karibuni.
Serikali ilimtuhumu kwa kuongeza chumvi msaada wake nchini humo na kutaka kushughulikiwa kama mtu muhimu sana.
Msimamizi mkuu wa Madonna, Trevor Neilson, alituhumu serikali kwa kuwa na kisasi na shirika la misaada la mwimbaji huyo, Raising Malawi.
Neilson pia aliwatuhumu maafisa wa serikali kwa kutumia vibaya pesa za zinazonuiwa kusaidia shule na hata kunyanyasa mashirika ambayo Madonna alikuwa ametoa msaada kwao.
0 maoni:
Post a Comment