MWANAHARAKATI WA MASHOGA MBALONI NCHINI ZAMBIA
Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja, amekamatwa nchini Zambia kwa kuonekana kwenye televisheni akitaka uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kutofanywa kuwa hatia.
Paul Kasonkomona alishatakiwa kwa kosa la ''kuwachochea watu kushiriki vitendo visivyokubalika,'' alisema mkuu wa polisi Solomon Jere.
Paul alikamatwa alipokuwa anaondoka nje ya studio hizo za kampuni ya kibinafsi ya Muvi.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ni haramu nchini Zambia.
Wadadisi wanasema kuwa watu wengi, wanaamini kuwa ni kinyume na imani zao Duru katika stesheni hiyo, mjini Lusaka zilisema kuwa polisi walijaribu kukatiza mahojiano lakini wakuu wa stesheni hiyo walikataa.
Katika ombi lililotolewa kwa rais wa Zambia Michael Sata, kundi moja la wanaharakati nchini Afrika Kusini Ndifuna Ukwazi, lilitaka kuachiliwa mara moja kwa bwana Kasonkomona.
Kundi hilo pia lilisema linataka serikali ya Zambia kuanzisha mara moja mpango wa kutofanya vitendo hivyo kuwa kinyume na sheria ikiwa itakuwa kati ya watu wazima licha ya jinsia yao.
Vitendo kama ulawiti na uhusiano wa mapenzi kati ya wanawake, vina adhabu ya miaka 15 au kufungwa maisha jela.
0 maoni:
Post a Comment