FBI
NDANI YA ARUSHA KUSAKA MAGAIDI
Kikosi maalumu cha FBI kutoka nchini Marekani wamewasili nchini Tanzania ili kusaidia katika upelelezi wa magaidi walioshambulia katika kanisa katoliki mjini Arusha mnamo majira ya saa tano asubui siku ya jumapili.
makachero hao wa FBI wako Tanzania kusaidiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi kutafuta undani wa tukio hili ambalo limeishtua na kuiweka serikali ya Tanzania katika wakati mgumu.
Wakati huo huo wakuu wa serikali wakishirikiana na viongozi wa kidini wameandaa mkutano utakaojumuisha viongozi wapatao 200.Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq amewaambia wanahabari kuwa wamelazimika kuandaa mkutano huo wa siku mbili kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo utajadili uhusiano bora baina ya wakrito na waislamu.
0 maoni:
Post a Comment