MATATU YA SOMALIA YAGOMA
Waendesha mabasi nchini Somalia wamegoma kwa siku ya pili kwa sababu wanasema inabidi wawalipe rushwa wanajeshi wa serikali na polisi katika vituo vya ukaguzi.
Madereva wa mabasi na malori mjini Mogadishu na miji mengine wamekataa kufanya kazi hadi swala hilo limeshughulikiwa.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia, AMISOM, kimeingilia kati kujaribu kutatua mkwamo huo.
Msemaji wa polisi ameiambia BBC kwamba wanachunguza malalamiko hayo lakini hawana habari kwamba askari polisi wanadai hongo
0 maoni:
Post a Comment