VIONGOZI WA AU, WAANZA MAZUNGUMZO.
Baada ya sherehe za Jumamosi mjini
Addis Ababa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, viongozi
wa Afrika sasa wanajadili baadhi ya matatizo yanayokabili bara hilo.
Vita vya muda mrefu katika Jamhuri
ya Demokrasi ya Congo vilichukua nafasi kubwa mazungumzo yalipoanza.
Tena majadiliano yakahusu pendekezo
la kuyafanya mahakama ya jinai ya kimataifa, ICC, yaache hatua za kumfikisha
mahakamani rais mpya wa Kenya na makamo wake kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya
binaadamu.
Wanabalozi wanasema viongozi wa
Afrika wamegawika kuhusu swala hilo.
Mawaziri wa Mashauri ya Nchi za Nje
walikubaliana Alkhamisi, kabla ya viongozi kukutana, kwamba AU iiombe ICC
kupeleka jukumu la kesi za Rais Uhuru Kenyatta na makamo wake Wiliam Ruto kwa
mahakama ya Kenya.
0 maoni:
Post a Comment