Mjumbe maalum wa Mwenyekiti wa Tume
ya Umoja wa Afrika (SRCC) nchini Somalia, Balozi Mahamat Saleh Annadif
ameshutumu vikali shambulio la kigaidi lililofanywa leo na magaidi wa
Al-Shabaab katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
"Tunalaani vikali shambulio
hili la kinyama katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu. Mashambulio
haya yasiyofanikiwa yanayoendeshwa na Al-Shabaab yanalenga tu kuvuruga jitihada
zinazochukuliwa na wananchi wa Somalia baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe
vilivyodumu kwa zaidi ya ishirini na magaidi hao hawawezi kuzuia jitihada zetu
za pamoja kuendelea kuwasaidia wananchi wa Somalia kuijenga nchi yao"
amesema Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika nchini Somalia
(SRCC), Balozi Mahamat Saleh Annadif.
Balozi Mahamet Annadif amepongeza
hatua ya haraka iliyochukuliwa na majeshi maalum ya AMISOM na majeshi ya usalama
ya Somalia na amesisitiza kuwa AMISOM haitaacha kuchukua hatua za kuimarisha
usalama nchini Somalia.
"Umoja wa Afrika na AMISOM kwa
sasa wako pamoja na wananchi wa Somalia," amesema Balozi Annadif, wakati
akituma salaam za rambirambi kwa wale waliowapoteza wapendwa wao katika
shambulio hilo na kuwaombea kupona haraka watu wote waliojeruhiwa.
Takriban watu 12 wakiwemo ria wa
kigeni wameuawa katika shambulizi baya lililofanywa dhidi ya ofisi ya umoja wa
mataifa mjini Mogadishu Somalia
Ufyatulianaji risasi uliodumu kwa
zaidi ya saa moja ulishuhudiwa ndani ya ofisi za shirika la maendeleo la umoja
wa mataifa UNDP.
Mpiga picha aliyeshuhudia kisa
hicho, aliambia BBC kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua ndani ya
gari moja liliokuwa karibu na lango kuu la ofisi hizo na kuwa aliona
washambuliaji wanne wakiingia ndani ya ofisi yenyewe.
Kundi la Al Shabaab limesema kuwa
ndilo lilifanya shambulizi hilo.
Maafisa wa usalama wameweza
kudhibiti eneo hilo kwa sasa.
Somalia haijakuwa na serikali
thabiti kwa zaidi ya miaka 20, na kipindi hicho chote nchi hiyo ilikuwa eneo la
vita.
Lakini sasa serikali inapata msaada
kutoka kwa umoja wa mataifa na imeweza kudhibiti miji mingi ya nchi hiyo na
hata kufurusha wapiganaji wa al-Shabaab.
Hata hivyo waziri mkuu Abdi Farah
Shirdon Saaid, amesema kuwa Al Shabaab haiwezi kushinda vita dhidi ya serikali
inayojaribu kuleta utulivu na amani nchini kote
Ofisi kuu ya shirika la UNDP, iko
karibu na eneo lenye ulinzi mkali karibu na uwanja wa ndege Kusini mwa
Mogadishu.
Baadhi ya wale waliouawa na
wafanyakazi wa UN, majengo pia yameharibiwa na watu wamelazimika kukimbilia
usalama wao.
0 maoni:
Post a Comment