Kinyang'anyiro cha
kuwania kombe la shirikisho la CECAFA au kilabu bingwa Afrika Mashariki na
kati, kinaanza leo katika jimbo la Kordofan Kusini licha ya kuwepo wasiwasi
kuhusu hali ya usalama.
Baadhi ya vilabu
vimegoma kwenda kwa michuano hiyo ikiwemo Yanga ya Tanzania wakieleza wasiwasi
kuhusu usalama wao kwenye michuano hiyo ambayo pia inachezewa katika jimbo la
Darfur.
Katibu mkuu wa CECAFA,
Nicholas Musonye, alikwenda Kordofan siku ya Jumapili na kukutana na maafisa
kutoka Khartoum waliohakikisha kuwa michuano inaendelea bila wasiwasi wowote.
Maafisa wamewataka
wananchi kuunga mkono michuano hiyo kwani usalama katika mviwanja vyote
umedhibitiwa vilivyo.
Nia ya CECAFA ni
kuonyesha kuwa maisha yanaendelea kama kawaida katika jimbo la Darfur na
Kordofan Kusini licha ya mgogoro unaoendelea katika maeneo hayo.
Lakini raia wengi wa
Sudan wameshangazwa sana na uamuzi wa michauano kuandaliwa katika majimbo hayo.
Moja ya viwanja ambako
michuano ya CECAFA itachezwa Kadugli
Musonye pia alisema
kuwa timu ya Al Nasr kutoka Sudan Kusini ilijaribu kubatili uamuzi wake wa
awali, kukosa kushiriki lakini ombi lao lilikuja kuchelewa.
Kwa sasa kuna mgogoro
mkubwa katika jimbo la Kordofan Kusini na katika mji mkuu wa jimbo hilo
Kadugli, ambako mechi ya ufunguzi itachezwa katika uwanja ambao umewahi
kushambuliwa kwa makombora mwaka uliopita.
Mzozo tofauti uliibuka
katika jimbo la Darfur mwongo mmoja uliopita, na eneo hilo bado lina makundi ya
watu waliojihami pamoja na makundi ya wapiganaji.
Mji mkuu wa jimbo la
Darfur Kaskazini, Fasher, ambao ni mwenyeji wa michuano kadhaa, ni makao kwa
kikosi cha umoja wa mataifa kinachoshirikiana na muungano wa Afrika ambao
wanajribu kuleta utulivu kwa eneo hilo.
Hata hivyo wakaazi wa
mji mkuu Kadugli wanajiandaa kwa mechi ya kwanza ya kimataifa kuwahi kufanywa
mjini humo.
Maafisa wa michuano
pamoja na marefa waliwasili Jumapili mwishoni mwa wiki na kumtembelea gavana wa
jimbo hilo, Ahmed Harun nyumbani kwake.
Musonye pia alikutana
na Harun pamoja na kamati ya maandalizi ya michuano hiyo.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment