Kocha wa timu ya Taifa stars, Kim Poulsen, ameita
tena kambini timu hiyo julai 4, mwaka huu ili kujiandaa na michuano ya kutafuta
tiketi ya kushiliki mwichuano ya fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani
itakayofanyika nchini Afrika Kusini.
Kikosi cha Taifa Stars kimevunja kambi leo mara
baada ya kucheza mchezo wa jana na timu ya Ivory Coast, Tanzania na Ivory Coast
wote wapo kundi C, katika michuano hiyo ambapo Vijana wa Stars alichezea
kichapo cha bao 4-2.
Wachezaji wote wataitwa kambini ispokuwa ni Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu, kutokana na kuwa michuano hiyo ni kwa wachezaji wa
ndani tu, hivyo basi hao wawili hawatokuwepo kutokana na kuwa wanachezea nje ya
nchi.
0 maoni:
Post a Comment