Maelfu ya watu nchini
Misri wameandamana mjini Cairo kumuunga mkono rais Mohammed Morsi.
Maandamano hayo
yaliandaliwa na chama cha rais Morsi cha Muslim Brotherhood kwa ushirikiano na
makundi mengine ya kiisilamu.
Waandamanaji walipiga
mayowe wakilaani walichokiita upinzani ambao unapanga maandamano makubwa mwezi
huu dhidi ya utawala wa rais Morsi.
Utakuwa ndio mwaka wa
kwanza tangu kuingia mamlakani kwa rais Morsi atakayetawala kwa miaka mitano.
Waandamanaji hao
wataandamana wakitaka kumshikiza rais Morsi.
Wadadisi wanasema kuwa
maandamano ya kumpinga rais Morsi pamoja na yale ya kumuunga mkono ni ishara ya
kuonyesha hali ya migawanyiko ilivyo kisiasa nchini Misri zaidi ya miaka miwili
baada ya mapinduzi ya kiraia kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.
kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment