CHRIS BROWN, AMEPEWA HUKUMU YA KUSAFISHA MAZINGIRA KWA MASAA 1,000.
Chris Brown, amehukumiwa na jaji hapo jana kutumikia jamii kwa muda wa masaa 1,000. Maamuzi hayo yalitolewa hapo jana katika mahakama moja huko mjini Los Angeles, kufuatia kuwa msanii huyo kuto fanya mambo aliyopangiwa.
CB, anatakiwa kusafisha mazingira mbalimbali ikifuatiwa na kazi nyengine atakazo pangiwa na idara ya probation.
Mama mzazi wa msanii huyo naye alikuwa mahakani hapo, kusikiliza kesi hiyo inayomkabili msanii huyo, ambaye hapo jana alionekana kuwa mwenye hasira sana.
0 maoni:
Post a Comment