Msanii wa muziki wa Bongo Feva nchini, DUDU BAYA,
amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi waliopotea kwenye Game wamekuwa na
Stress za Muziki ambazo zinawaumiza wasanii wengi ambazo zinawapelekea kunywa
pombe, kuvuta Bangi na mwishowe kutumia madawa ya kulevya.
Dudu Baya, alisema kuwa yeye ategemei mziki tu bali
pia ni mjasiliamali, mpaka sasa ameweza kuwa na Kampuni Zake Ikiwemo ya Mbao huko mjini
Mwanza, Mambas Timber, Mambas Entertainment
, na Mambas Pub,iliyoko jijini Dar es salaam, ndivyo vitu peke vinavyofanya maisha yanasonga mbele, hayo
aliyasema alipofanyiwa mahojiano na mtandao wa Bongo5.
Achiliambali usanii wake wa kuimba muziki pia yeye
ni Mchoraji wa Ramani za majumba na Fundi pia, alisema kuwa kwa wasanii
waliochoka na maisha awape kazi katika kampuni zake hizo, hayo ni maneno ya
Dudu Baya.
0 maoni:
Post a Comment