Maseneta wawili wa Marekani John McCain na Lindsey Graham wamewasili
mjiniCairo, wakati jitihada zikishika kasi kuutatua mzozo wa kisiasa nchini
Misri uliozuka baada ya kupinduliwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed
Morsi.
Wasiwasi unazidi
kutanda baada ya serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi kutangaza mpango mpya
wa kuyasitisha maandamano, ambako wafuasi wa Morsi wanataka arudishwe
madarakani.
Katika siku za hivi
karibuni kumekuwa na wageni mashuhuri wa kiimataifa wanaozuru Misri,
wanaotarajia kusaidia kusimamia kupatikana suluhu ya amani katika hali ya
suitofahamu iliopo kati ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa na serikali
inayoungwa mkono na jeshi.
Lakini mpaka sasa
hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu hatua zilizopigwa.
Kwa wakati mmoja
kulikuwa na ripoti kwamba baraza jipya la mawaziri lilikuwa tayari kuwaachia
viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood kutoka gerezani na kuwapatia
nyadhifa za mawaziri iwapo watasitisha maandamano mjini Cairo.
Hata hivyo mshauri wa
rais amekana tuhuma hizo na wafuasi wa Morsi wamesisitiza hawatokubali chochote
isipokuwa kurudishwa Morsi madarakani.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment