Mfalme wa Morocco amebatili uamuzi wake wa kumsamehe mwanamume raia wa
Uhispania aliyeshtakiwa kwa kuwaharibu watoto 11 walio kati ya umri wa miaka 4
na 15. Hii imethibitishwa na maafisa kutoka kasri la mfalme Mohammed wa sita.
Inaarifiwa mfalme
hakuwa na uelewa wa ukubwa wa kosa alilofanya raia huyo mhispania kulingana na
baraza lake la mawaziri kabla ya kuwasamehe wafungwa.
Mshukiwa huyo alikuwa
miongoni mwa watu 48 raia wa Uhispania walioachiliwa huru kufuatia msamaha wa
Mfalme , hali iliyosababisha maandamaano makubwa mjini Rabat siku ya Ijumaa.
Waandamanaji
walitishia kufanya maandamano mapya mjini Rabat na Casablanca wiki ijayo.
Daniel Galvan Vina,
anayeaminika kuwa na umri wa miaka sitini, alihukumiwa jela miaka 30 tangu
Septemba mwaka 2011.
Hata hivyo, wiki jana
, aliachiliwa baada ya mfalme kuamuru kuwa wafungwa waachiliwe kutoka jela la
Kenitra, Kaskazini mwa mji mkuu Rabat. Inasemekana kuwa mtu huyo tayari
ameondoka nchini.
Hata hivyo wizara ya
sheria imesema kuwa itajadili hatua itakazochukua kutokana na raia huyo wa
Uhispania.
Mamia ya watu
walijeruhiwa katika makabiliano yaliyozua ghasia kati ya waandamanaji na polisi
nje ya bunge la nchi hiyo siku ya Ijumaa.
Maandamano pia
yaliripotiwa kufanyika katika miji ya Kenitra, Tangier na Tetouan, pamoja na
nje ya ubalozi wa Morocco mjini Paris.
"mfalme hakuwahi
kufahamishwa chochote kuhusu kesi hiyo, na mashtaka aliyokabiliwa nayo mtu huyo
kiasi cha kufungwa jela, '' ilinukuu taarifa kutoka kwa Ikulu ya Rais mnamo
Jumapiali.
Ni jambo la kawaida,
kwa mfalme kuwasamehe wafungwa kwa kipindi maalum kama wakati wa sherehe za
siku ya kutawazwa ufalme iliyoadhimishwa Jumanne iliyopita.
Waziri wa sheria wa
Morocco, alisema Ijumaa kuwa msamaha ulitolewa kwa sababu za kitaifa na
uhusiano mzuri na Uhispania.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment