kumbe msanii wa Bongo Fleva, Diamond naye alikuwa katika Abiria walioshukia nchini Kenya, hawa ndiyo Abiria wakipelekwa katika Hoteli iliyoko Nairobi Kenya.
mara baada ya kupona katika tukio hilo msanii huyo DIAMOND , alifunguka katika Mtandao wake wa Habari kwa kusema (Kiukweli ni jambo la kumshukuru Mungu kwangu mimi na Abiria
wote kutuepushia na mabalaa yoyotetangu mwanzo wa safari hadi hapa tulipo na Mwenyezi Mungu
akasimame nasi kutufikisha nyumbani salama...)
========================================================================
Moto mkubwa umetokea katika uwanja
wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta ulioko jijini nairobi. Kwa sasa moto huo
umeweza kudhibitiwa
Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika
uwanja huo na anatarjiwa kuhutibia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia
sasa hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema
kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia
wageni.
Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa
tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.
Imesema kuwa baadhi ya operesheni za
uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa
kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali,
Mombasa na kwingineko nchini Kenya.
Baadhi ya safari za ndege kutoka
uwanja huo pia zime-ahirishwa.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment