Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi
Kagasheki ametangaza nia ya kujiuzulu wadhifa wake dakika chache zilizopita
bungeni mjini Dodoma,sababu kubwa ya
kujiuzulu ni baada ya kusomwa ripoti ya
kamati ya Bunge Kumtuhumu kuzembea na kukithiri kwa vitendo viovu vilivyofanywa
na wanausalama wakati wa Operesheni Tokomeza.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira
imebainisha kuwa oparesheni Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa na Serikali
ilikumbwa na unyanyasaji mkubwa wa wananchi, Ukatili, Udharirishaji, Ubakaji na
Mauaji huku baadhi ya wazazi wakivuliwa nguo, kuteswa na kubakwa mbele ya
wanafamilia.
Akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo Mwenyekiti
wake James Lembeli amesema pamoja na mateso hayo yaliyowakumba wananchi pia
nyumba zao zilichomwa na mifugo kupigwa risasi huku mingine ikifa kwa kukosa
maji, chakula na maziwa kwa ndama wadogo.
Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa vitendo vya
Rushwa vilivyotawala oparesheni Tokomeza ambapo pia wananchi waliokuwa na
mifugo walitozwa faini na mifugo mingine kuuzwa kwa bei nafuu ambayo
haikulingana na faini iliyokuwa ikitoza na wafugaji walizuiwa kushiriki mnada
wa uuzaji wa mifugo hiyo.
[Taarifa kutoka kwa millard ayo]
[Taarifa kutoka kwa millard ayo]
0 maoni:
Post a Comment