Mandela daima alisema anataka kuzikwa nyumbani alikozaliwa Qunu |
Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela,
kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba
za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka
hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali
ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege
, kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati
huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika
kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia
alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano
uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa
huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990
alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni
mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa
vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika
pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira
aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa
pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili
kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.
Mazishi ya Mandela yatafanywa kuambatana na tamaduni za watu wa Xhosa |
0 maoni:
Post a Comment