Bado haki za marehemu Sharo Milionea zinazidi kumtesa
mama yake mzazi, Zainabu Mkiety ambaye ameendelea kulalamika kuwa watu
wanaopaswa kuzilipa wamejikausha!
Kwa mujibu wa Global Publishers, mama Sharo amesema
watu ambao walikuwa wanadaiwa na Sharo kupitia kazi ambazo alizifanya
wamenyamaza bila kumwambia nini kinachoendelea.
Mama Sharo amesema hakuna alichoambulia zaidi ya fedha
za gari alilokuwa anatumia marehemu pamoja na vitu vya ndani.
“Nawaomba wasinidhulumu jamani, nahangaika na uzee
huu, mwanangu alikuwa ndiye nguzo maishani mwangu, mfano niliona hadi kalenda
lakini sikuona chochote juu ya kalenda hizo, nawaomba sana,” mama Sharo
amemwambia mwandishi wa Global Publishers.
0 maoni:
Post a Comment