Klabu Tottenham imemtimua kocha wake Andre Villas Boas
siku moja baada ya Tottenham kupata kichapo cha magoli 5- 0 kutoka Liverpool
Kipigo hicho cha magoli 5 - 0 ni moja kati ya matokeo
mabaya kutokea katika uwanja wao wa nyumbani wa Tottenham wa White Hart Lane kwa takriban miaka 16
iliyopita.
Wakati Tottenham wakitimua kocha kwa upande wake
Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers amesema hatua ya timu yake kuisambaratisha
Tottenham kwa magoli 5 - 0 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane ni moja kati ya mechi
ya viwango vya juu vilivyoonyeshwa na Liverpool
katika kipindi cha uongozi wake.
Rodgers alishika hatamu ya kuinoa Liverpool mwaka 2012
ambapo kwa sasa timu hiyo ipo nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Arsenal katika
msimamo wa ligi kuu ya England.
"Ni matokeo mazuri na viwango vya hali ya
juu," amesema Rodgers.
"Tumepata magoli matano na inawezekana tungepata
mengi hata saba au nane. Huo ndio uzuri wa timu ambapo inapata magoli."
Mshambuliaji wa timu hiyo Luis Suarez alifunga magoli
mawili wakati Jordan Henderson, John Flanagan na Raheem Sterling wakifunga kila
mmoja.
Wakati wa mchezo huo Tottenham alishindwa kulenga hata
mara moja kwenye goli la Liverpoool ambayo imefunga timu hiyo katika mechi nane
za ligi kuu ya England
ziliyochezwa kwenye kiwanja hicho.
0 maoni:
Post a Comment