Mapigano makali yanaendelea Sudan Kusini, baina ya
wanajeshi wa serikali ya Rais Salva Kiir, na wale watiifu kwa makamo wa rais wa
zamani, Riak Machar.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Hilde Johnson,
anasema watu zaidi ya elfu moja wameuwawa, ingawa idadi hasa haijulikani.
Viongozi wa Afrika wanajaribu kupatanisha na Rais
Salva Kiir amekutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, na waziri mkuu wa
Ethiopia, Hailemariam Desalegn.
Ripoti zinasema viongozi hao wamejadili juu ya
uwezekano wa kusitisha mapigano, mazungumzo ya kutafuta amani, na maafa ya raia
hivi sasa.
Haijulikani kama viongozi wa Ethiopia na Kenya watakutana na Bwana Riek
Machar piya.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi
anaeleza kuwa Sudan
Kusini ni muhimu kibiashara kwa jirani zake.
Kenya imeiuzia
nchi hiyo bidhaa za thamani ya dola 290 milioni mwaka huu.
Serikali ya Kenya
inasema raia wake kama 1,000 bado wamenasa katika miji ya Sudan Kusini -
wafanya-biashara, walimu, wafanyakazi katika usalama na wachuuzi.
Piya kuna wasiwasi kuwa mapigano yakizidi
yataakhirisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini hadi
bandari ya Lamu, Kenya.
0 maoni:
Post a Comment