Aliyekuwa waziri wa fedha wa Lebanon
Mohamad Chatah ameuawa kwa bomu mjini Beirut.
Watu wengine wane waliuawa na takriban Watu 50 wamejeruhiwa katika shambulio linalokisiwa kuwa la bomu lililotegwa kwenye gari.
Chatah,muislamu
wa jamii ya Sunni alikuwa mshauri wa Waziri mkuu wa zamani Saad Hariri.pia
alikua mkosoaji mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad na chama cha
Hezbollah kilichokua kikimuunga mkono Assad.
Kumekuwepo na wimbi la mashambulizi Lebanon,yanayohusishwa na jamii ya Sunni na Shia hasa kuhusu mapigano ya Syria.
Saad Hariri alikuwa akishutumu chama cha Hezbollah kufanya mashambulizi nchini humo.
Watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Hezbollah wanatarajiwa kufikishwa mahakamani majuma matatu yajayo wakishutumiwa kushiriki mauaji ya Baba wa Saad Hariri na aliyekuwa Waziri Mkuu Rafik,waliouawa kwa shambulio la bomu mwezi Februari mwaka 2005.
Chama cha Hezbollah kimekana kuhusika na kifo cha Rafik Hariri.
kutoka BBC-Mweraamazing
0 maoni:
Post a Comment