Msanii wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili, amekanusha
kutoa wimbo uliovujishwa na watu, “ Ngalelo” kuwa wimbo huo ulikuwa ni
freestyle tu.
“Kuna wimbo nimeona wametoa toa kwenye mablog
wameandika kwamba nimetoa wimbo wangu mpya, of course huo sio wimbo. Kuna
studio nilikuwa nimeenda nikafanya freestyle tu inaonekana hao jamaa
wameivujisha.” Nikki wa Pili ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Ni ile ile (studio) ya Afro Centric lakini ni
producer mwingine na sio producer ambaye yuko sasa hivi. Ni kule maeneo ya
Hostel karibu na chuo kwa hiyo nilikuwa na shindashinda hapo, hayo yalisemwa na
msanii huyo, pia aliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya mistari imetumika katika
baadhi ya nyimbo zake.
0 maoni:
Post a Comment