
Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Nay wa Mitego,
amefunguka na kusema kupitia kipindi cha Bongo
Dot Home ya 100.5 Times Fm
kuwa kitendo alichokifanya Ostaz Juma kupost picha zinazomuoenesha PNC
akimpigia magoti, kwa upande wake amemkosea yeye hata kuliko PNC mwenyewe.”............
Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja, hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo. Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.”

0 maoni:
Post a Comment