MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

OSCAR PISTORIUS, AKANUSHA MASHTAKA



 
Mwanaridha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amekanusha mashitaka ya kumuua mpenzi wake wakati kesi yake ikianza mjini Pretoria............


Pistorius ambaye ana ulemavu wa miguu na ambaye hutumia miguu bandia ameshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake na mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Oscar amesema alimpiga risasi marehemu kimakosa kwani alidhani alikua mwizi.

Mahakama mjini Pretoria ilimuachilia Pistorius kwa dhamana ya randi millioni moja, sawa na kiasi ya Dola laki moja.

Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentines mwaka jana.

Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment