Waziri Mkuu wa Uchina, Li Keqiang, na viongozi wa
Afrika Mashariki wametia saini rasmi makubaliano ya kujenga njia mpya ya reli
itayounganisha mji wa Kenya wenye bandari, Mombasa, hadi Nairobi, Rwanda na Sudan Kusini............
Waziri Mkuu wa Uchina yuko mjini Nairobi akiwa katika ziara ya Afrika.
Njia hiyo ya reli ya upana unaotumika kawaida duniani
itagharimu mabilioni ya dola, na itachukua nafasi ya njia ya reli ya sasa
ambayo ni nyembamba na ilijengwa zama za ukoloni wa Uingereza.
Sehemu ya kwanza ya reli itajengwa na kampuni za
Uchina - jambo lilozusha malalamiko kwamba kampuni nyengine hazikuruhusiwa
kushiriki katika kuomba kandarasi.
Chanzo BBC.
0 maoni:
Post a Comment