MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

EWURA YATANGAZA BEI MPYA YA MAFUTA (JANUARI 06, 2014)

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la Ulaya.................

                    
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.

Alisema kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.311 kwa lita.

Alisema bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.

Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.

Alisema katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na karibu asilimia 40.

Alisema viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za usafirishaji.

Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa risiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.

"Natoa wito kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa risiti kwani itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.

Naye Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri kuhakikisha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.


Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo haitajitokeza.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment