Kumeripotiwa tetemeko jingine lenye nguvu
nchini Nepal siku moja baada ya tetemeko kubwa lililosabaisha vifo vya karibu
watu 2000............
Watu
walikimbia kwenda maeneo ya wazi kwenye mji mkuu wa Kathmandu wakati
kulipotokea tetemeko hilo la vipimo vya 6.7 na kutikisa majengo.
Tetemeko
hilo nalo lilisikika kaskazini mwa India na Bangaldesh na kusasababisha
maporomoko ya theluji katika mlima wa Everest.
Ndege
za misaada , madaktari na watoa misaada kutoka nchi jirani zimeanza kuwasili
nchini Nepal.
Ndege
kutoka India na China zimetua mjini Kathmandu kusaidia katika jitihada za
uokozi.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment