Tetemeko
kubwa la ardhi limekumba eneo lililo magharibi mwa Nepal karibu na mji mkuu wa
Kathmandu .Maafisa wa polisi wanasema kuwa zaidi ya watu 560 wamethibitshwa
kufariki huku wengi wakiwa hawajulikani waliko na kwamba huenda idadi hiyo
ikaongezeka...............
Shirika la utafiti la
Marekani liliseme kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo lililo
umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara magharibi mwa mji mkuu wa
Kathmandu
Kuna ripoti za
uharibifu wa majengo. Idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa haijulikani.
Picha za majengo
yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana
kwenye mitandao ya kijamii.
Mawasiliano ya simu
nayo yameharibiwa.
Walioshuhudia walisema
kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Mitetemeko mingine
midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan.
chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment