Watu wapatao 3,617 wamefahamika kufa
katika tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga Nepal Jumamosi...........
Kituo
cha Taifa cha Dharura cha Majanga kimesema watu zaidi ya 6,500 wamejeruhiwa.
Watu
kadhaa pia wameripotiwa kufa katika nchi jirani za China na India
Zaidi
ya wapanda milima 200 wameokolewa kuzunguka Mlima Everest, ambao umekumbwa na
athari za tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8.
Wakaazi
wengi wa mji mkuu Kathmandu wamekuwa wakilala katika mahema kwa wale wasio na
makazi au wanaohofia kurudi majumbani kutokana na athari zaidi za tetemeko la
ardhi zinazoendelea. Maelfu wamelala nje kwa siku ya pili Jumapili, baada ya
tetemeko hilo kuipiga Nepal Jumamosi.
Maafisa
wamesema idadi ya vifo au majeruhi ikaongezeka wakati huu ambapo vikosi vya
waokoaji vimefanikiwa kufika katika ameneo ya milimani magharibi mwa Nepal.
Taarifa
za awali zinasema jamii nyingi za watu, hususan wanaoishi karibu na kingo za
mlima, wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na tetemeko hilo.
Mtu
mmoja ambaye aliokolewa na helikopta kwenda katika mji wa Pokhara, kilomita 200
kutoka Kathmandu, amesema karibu kila nyumba katika kijiji chake chenye nyumba
zaidi ya 1,000 kimeharibiwa, Bwana Darvas ameiambia BBC.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment