Mkuu
wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Hussein, amekuwa
akifadhaishwa sana na lugha ya magazeti ya Uingereza wanayotumia dhidi ya
wakimbizi, lakini ni taarifa ya hivi punde iliyochapishwa na makala ya
‘The Sun’
iliyomghadhabisha zaidi..............
Makala hiyo iliwaita
wakimbizi mende, matamshi ambayo Hussein anasesema ni sawia na yale yaliotumika
Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari.
Mkuu huyo wa Haki za
Kibinadamu amesema taarifa hiyo ya The Sun ilikuwa mojawapo tu ya taarifa
nyingi za chuki na za kibaguzi ambazo zimechapishwa kwa miongo mingi na
magazeti ya Uingereza.
Alisema desturi hii
ilikuwa inaongeza moto wa chuki na udhalilishaji wa binadamu wengine. Hussein
alisema kuwa malalamishi kuhusu makala hizo tayari yamepelekwa kwa Polisi wa
jiji na akataka kuchukuliwe hatua kali.
Matamshi haya, hasa
kutoka kwa afisa wa juu sana wa umoja wa mataifa, umeashiria
wasiwasi ulioko
kuhusu mjadala unaoendelea bara Uropa kuhusu wakimbizi wanaovukia Meditteranean
kuingia Ulaya .
Mjadala ambao
unasemekana unaendeshwa na hisia kali kwenye vyombo vya habari, na kwamba maoni
ya uma huenda hayaungi mkono hatua zinazohitajika kuokoa maisha ya wanaokufa
maji huko mediterrenean
chanzo ni BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment