Baba wa mtoto kutoka
nchini Syria ambaye alikufa maji wiki hii na kuzua changamoto za kutaka
kuchukuliwa hatua za kutatua suala la uhamiaji nchini syria anaripotiwa kukataa
hatua ya Canada ya kumpa makao.
Tima Kurd, ambaye ni
dadake Abdullah al Kurdi alisema, alimuambia kuwa anataka
kusalia nchini Syria
yaliko makaburi ya mkewe na wanawe wawili wa kiume ambao pia walikufa maji nje
ya pwani ya Uturuki siku ya jumatano.
Wote hao walizikwa
nchini Syria siku ya Ijumaa
Picha za mwili wa mtoto
huyo wa miaka mitatu katika ufuo wa Uturuki zilizua mjadala kuhusu hatma ya
watu wanaokimbia mapigano nchini Syria.
{chanzo bbc}
0 maoni:
Post a Comment