Urusi imeanza kufanya
mashambulizi ya anga dhidi ya wanaompinga rais wa Syria Bashar al-Assad.
Mashambulizi
yameripotiwa kulenga maeneo yanayodhibitiwa na waasi ya miji ya Homs na Hama na
kusababisha madhara.
Marekani imesema
ilipatiwa taarifa hizo saa moja kabla ya mashambulizi kutekelezwa.
Maafisa wa ulinzi wa
Urusi wamesema wamekuwa wakiwalenga wanamgambo wa Islamic State, lakini maafisa
wa Marekani wamesema mashambulizi hayo hayakuonekana kulenga ngome ya IS.
Marekani na washirika
wake wamekuwa wakisisitiza kuwa Rais Bashar al-Assad aachie madaraka, huku
Urusi imekuwa ikimuunga mkono Assad kuendelea kubaki madarakani.
Waziri wa mambo ya nje
wa Marekani John Kerry amesema nchi yake ilikua imejiandaa kuunga mkono hatua
za kijeshi za Urusi lakini iwapo tu Operesheni zake zitakuwa dhidi ya makundi
ya IS na al-Qaeda.
Chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment