Wanasiasa saba
waandamizi wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka kutokwamilia
madaraka, kulingana na maafisa.
Katika barua kwa Joseph
Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya muungano huo lilitaka hatua
kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kufikia mwezi Novemba.
Mda wa kikatiba wa rais
Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania
muhula mwengine.
Upinzani pia unahofia
kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa.
Ulifanya mkutano wa
kisiasa katika mji mkuu wa Kinshasa hapo siku ya jumanne ili kumtaka rais
Kabila ajiuzulu mwaka ujao.
Msemaji wa serikali
Lambert Mende alikana kwamba bwana Kabila alitaka kukiuka katiba kulingana na n
chombo cha habari cha Reuters.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment