Japan na Korea Kusini
zimefikia makubaliano ya kihistoria kuhusu wanawake waliolazimishwa kuhudumu
katika madanguro kama watumwa wa ngono wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Japan imeomba msamaha
na kukubali kulipa yen 1bn ($8.3m, £5.6m) ambazo zitawekwa kwenye hazina ya
waathiriwa itakayosimamiwa na Korea Kusini.
Mzozo huo umeathiri
uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, Korea Kusini ikitaka kuombwa msamaha “kwa
dhati” na kutolewa kwa fidia kwa waathiriwa.
Mwafaka wa sasa ndio wa
kwanza kuhusu suala hilo tangu 1965 na umepatikana baada ya pande zote mbili
kuahidi kuharakisha mazungumzo.
Tangazo hilo limetolewa
baada ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Japan Fumio Kishida kuwasili Seoul kwa
mashauriano na mwenzake Yun Byung-se.
Baada ya mkutano
Kishida aliambia wanahabari kwamba Waziri Mkuu Shinzo Abe ameomba msamaha
kutoka kwa “wote walioathirika”.
Wanawake takriban
200,000 walilazimishwa kuwa watumwa wa ngono kwa wanajeshi wa Japan wakati wa
Vita Vikuu vya Pili vya DUnia, wengi wao wakitoka Korea.
Ni 46 pekee kati yao
walio hai Korea Kusini.
Wengine walitoka
Uchina, Ufilipino, Indonesia na Taiwan.
Japan ilikuwa awali
imekubali lawama kwenye taarifa iliyotolewa 1993 na katibu wa baraza la
mawaziri wa wakati huo Yohei Kono.
Hazina ya kibinafsi
ilianzishwa 1995 kwa ajili ya waathiriwa na ikadumu kwa mwongo mmoja.
Pesa hizo hata hivyo
zilitoka kwa michango ya wahisani na si kutoka kwa serikali ya Japan.
Kutoka BBCSwahili
0 maoni:
Post a Comment