Majeshi ya Iraq yamesema kuwa yanakaribia kuukomboa
mji wa Ramadi baada ya kuanzisha mashambulizi makali dhidi ya wapiganaji hao wa
IS waliokuwa wakishikilia mji huo tangu mwezi mei mwaka huu.
Maafisa wa vikosi vya serikali ya Iraq wanasema kuwa
hadi sasa wamefanikiwa kuzikomboa wilaya kadhaa mahala ambapo mamia ya
wanadhaniwa kuwepo.
Balozi wa Iraq nchini Marekani Lukman Faily
ameiambia BBC majeshi ya serikali na washirika wake walikuwa katika hatua za
mwisho za kushinda vita hivyo vya kuukomboa mji huo.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani Colonel
Steve Warren amekaririwa akisema kuwa bado kuna kazi kubwa katika mapigano hayo
dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
kutoka BBCSwahili.
0 maoni:
Post a Comment