Serikali ya Gambia
imepiga marufuku wafanyakazi wa kike kufika kazini wakiwa hawajajifunika
nywele.
Kupitia barua
iliyofichuliwa na magazeti ya kibinafsi nchini humo, serikali ya nchi hiyo
inasema wanawake lazima "wafunge nywele zao na kitambaa'' barua hiyo
haikutoa sababu yoyote ya kupiga marufuku.
Mwezi uliopita, Rais wa
Gambia Yahya Jammeh alitangaza nchi hiyo yenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya
Kiislamu.
Jammeh atangaza Gambia
kuwa nchi ya Kiislamu
Aliongezea kuwa watu
wasio Waislamu hawangelazimishwa kuvalia mavazi ya Kiislamu.
Gambia ni maarufu sana
kwa watalii kutoka magharibi kutokana na fukwe zake.
Mwaka 2013, Rais Jammeh
aliondoa taifa hilo kutoka kwa Jumuiya ya Madola akisema muungano huo wa
Uingereza na mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza ni ukoloni mamboleo.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment