Washirika kadha wa
Saudi Arabia wamejiunga na taifa hilo katika kuvunja uhusiano na Iran huku
mvutano ukizidi kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia.
Mataifa hayo ni
Bahrain, Sudan na Jumuiya ya Milki za Kiarabu (UAE).
Saudi Arabia ilikuwa
imewapa wanabalozi wa Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia
mvutano uliotokana na kuuawa kwa mhubiri maarufu wa Kishia.
Bahrain, ambayo
hutawaliwa na Mfalme Msuni lakini raia wengi ni wa dhehebu la Shia, nayo
ilifuata wa kuvunja uhusiano.
Ufalme huo pia uliwapa
wanabalozi wa Iran saa 48 wawe wameondoka nchini humo.
Sudan nayo ilimfukuza
balozi wa Iran kutoka Khartoum huku UAE nayo ikipunguza idadi ya maafisa wa
ubalozi. Waislamu wengi nchini Sudan ni Wasuni.
Taarifa ya wizara ya
ammbo ya nje ya Sudan imesema: "Kufuatia mashambulio ya kikatili dhidi ya
ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran na afisi yake ya ubalozi Mashhad... Sudan
inatakaza kwamba imevunja uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
Mhubiri huyo Sheikh Nimr
al-Nimr aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa
yanayohusiana na ugaidi.
Washia walishutumu
hatua hiyo na maandamano yalishuhudia maeneo yenye Washia wengi.
Mjini Tehran, waandamanaji waliteketeza majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment